Namuona Yeye
Mlango ni Mmoja tu-Wakuingia
Gusa unate- Utasimulia
Kuchoma,Kuvuta,Kunusa kujidunga Kijiko kigae
Unafikiri ni za mahohe-Hahe
Ni za brothers and sisters wale wajanjez
Namaanisha wale wajanja Mpaka wakapitiliza
Ujanja mwingi mbele kiza
Ni kizaa zaa, Mzozo Gumzo Gumzo la mtaa
Wale vijana smart and Talented ndo drug addicted
Wasambazaji tunawajua Hatutaki picha zao Mtaani ati Most Wanted
Hao ni not wanted Dead or alive
Wananifanya naona wababe wamekua wanyonge
Flani na flani wamekua wasenge
Nikiuliza naambiwa niache Wenge
Siach wenge
maana namuona Namuona-namuona
Namuona yeye akila Unga
-Matei Babu 2016