KITABU

Umewahi kujaribu, Kuwa na chako kitabu?
Kikiwa kwa taratibu, Kwa yale yalowasibu?
Chenye mengi majaribu, Chenye kutaka jawabu?
Watu wakawa karibu, Kujuwa yaliyosibu?

Waliokuwa waarifu, Walipataje adhabu?
Je wale wadanganyifu, Hawakupata aibu?
Wale ni waadilifu, Ni ipi yao swawabu?
Waliokuwa na bifu, Je walikuwa karibu?

Wasiokuwa na jiko, Walipata tabibu?
Wale wenye miamko, Hawakwenda kwa Zabibu?
Je wale wenye vituko, Waliishiwa sababu?
Wale wenye midundiko, Walikosa taarabu?

Wale wenye maswahibu, Walipata zipi tabu?
Asiefanya wajibu, Alitoa lipi jibu?
Imani ya Kuwa babu, Ilifika kwa katibu?
Wenye ustaarabu, Hawakupata ghadhabu?

Wale ambao ni wakali, Je waliweza kujari,
Wenye zao fahari, Mungu walimtafakari?
Wale wenye kujivinjari, Haukuwepo ushari?
Wauza medali, Je zililudi shekeri?

Hicho ni chako kitabu, Kikiwa na maajabu,
Kikionyesha adabu, Kufanya uwe dhahabu,
Ukipiga hesabu, Wengi utaweza tibu,
Kupata yao majibu, Kujenga waloharibu.

This poem is about: 
Our world

Comments

Additional Resources

Get AI Feedback on your poem

Interested in feedback on your poem? Try our AI Feedback tool.
 

 

If You Need Support

If you ever need help or support, we trust CrisisTextline.org for people dealing with depression. Text HOME to 741741