UZAZI

Mda ule wa gizani, Mtoto haonekani,
Watu wako mlangoni, Kufahamu jinsi gani,
Mwezi huoni gizani, Hawana matumaini,
Wamekaa nje ndani, Zidi kuimba vinywani.

Jua kutoka angani, Kilio chatoka ndani,
Dume kuja duniani, Shangwe toka midomoni,
Furaha masikioni, Baba wa thamani,
Mama kazimia, Hajui jinsi gani.

Wakunga wako usoni, Sheria zi mikononi,
Mtoto hamfanani, Kiuzito na usoni,
Ni Albino jamani, Wala hana thamani,
Mkinga hana utani, Mambo ya utamaduni.

Siri ipo hadharani, Furaha zero moyoni,
Maisha yapo matatani, Kifo kipo mlangoni,
Miezi yote tumboni, Hatakiwi duniani,
Kweri hawana imani, Ni Kweri hawana fani?

Mzazi tu haueni, Mtoto yu mashakani,
Kabla ya kwenda juani, Huuliwa kibandani,
Ukiwa tu mpinzani, Mkinga au ulizini,
Mama anamtihani, Nani atamuamini?

This poem is about: 
Our world

Comments

Additional Resources

Get AI Feedback on your poem

Interested in feedback on your poem? Try our AI Feedback tool.
 

 

If You Need Support

If you ever need help or support, we trust CrisisTextline.org for people dealing with depression. Text HOME to 741741