HUNTER VIRUS NA CORONA

Hunter virus na Corona, Tumekuja kwa maana,
Shetani si muungwana, Afanya yawe mapana,
Msahau Maulana, Mpate zake laana,
Wivu mkishikamana, Na mkisaidiana.

Yu anafanya uhuni, Watu wako majumbani,
Ataka wajaribuni, Msiende darasani,
Msiende makazini, Uchumi uwe gizani,
Ili mfeli shuleni, Mkate matumaini.

Elimu ya Maanani, Wafata ya duniani,
Ambayo ni ya mbinguni, Mtailudia lini?
Rudini kwenye dini, Hebu hata shtukeni,
Sie twawakumbusheni, Dunia iko mwishoni.

Twapita tu njiani, Ili tuwatisheni,
Tokeni dhambini, Rudini kwenye imani,
Elimu i hadharani, Ipendeni moyoni,
Dawa hio chukueni, Ya swala na Quran.

This poem is about: 
Our world

Comments

Additional Resources

Get AI Feedback on your poem

Interested in feedback on your poem? Try our AI Feedback tool.
 

 

If You Need Support

If you ever need help or support, we trust CrisisTextline.org for people dealing with depression. Text HOME to 741741