Akili ya mfungwa

Nimejipata mashakani baada ya Hakimu kuniukumu
maisha gerezani na majukumu ya kazi
ngumu
Tumeingishwa kwenye basi ambayo imetungoja pembeni
Ndani tuko wafungwa watano ilhali tumetwikwa kijiweni
Akuna anenaye kila kiumbe kimekimya kama bubu
Mchanganyiko ya wale hawana makosa na pia wezi sugu
Wengine ni macho chongo vichwani kuna ishara za
nundu
Alama kadhaa za visu usoni zile zimeshonwa kama
viraka
Michoro za nyusi na sindano wanapolea kama
mipira,duh!
Hofu inaninyemelea akilini sina amani
Story za gerezani zinaweza fanya nijirushe kisimani
Nguvu tayari imeninywea mapepo zimeanza kunisomea,
Natamani ningekua chuma ju afadhali ningechomelewa
Hila mimi ni binadamu maisha huru tayari ishanipotea
Sijui kama nitafika mwisho, sababu ni juu la kaa la moto
mahali natembelea,
Kisha..
Lango nene linafunguliwa na askari wenye mtutu
Pembezoni usalama umeimarishwa na sura zilizo tukutu
Hali ya anga bin vuu imebadilika ni kama tumefika
AKHERA!
"Harakishine hizo mikundu tayari mmefika Shimo la Tewa

This poem is about: 
Me

Comments

Additional Resources

Get AI Feedback on your poem

Interested in feedback on your poem? Try our AI Feedback tool.
 

 

If You Need Support

If you ever need help or support, we trust CrisisTextline.org for people dealing with depression. Text HOME to 741741